Fikia Upeo Company Limited

Usajiri wa Kampuni

Kampuni imesajiriwa Brela chini ya sheria ya usajili wa Makampuni na majina ya biashara.

Makao makuu ya Ofisi yapo Bariadi mkoani Simiyu. 

Unachohitaji kujua kuhusu kampuni yetu

Miliki kuu (Real Estate) ni moja kati ya sekta muhimu katika jamii maana inahusu ardhi na nyumba. Sisi, Fikia Upeo tumechukua jukumu la kuwekeza, kutoa elimu na kuonyesha fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye sekta ya Milki kuu (Real Estate). Kwa hiyo, kwa uzoefu tulionao wa zaidi ya miaka 10 katika sekta hii, tunaamini tunakitu cha kuipatia jamii kuhusu miliki kuu. Japo sekta hii ina changamoto nyingi lakini  ina fursa nyingi pia.

Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na;- Migogoro ya umiliki wa ardhi, changamoto za ujenzi na usimamizi wa nyumba, changamoto za uhaba wa elimu ya pango la ardhi/nyumba n.k.

Aidha zipo fursa lukuki za kibiashara kwenye sekta hii wale wanaozitumia, wengi wao hupata mafanikio makubwa kiuchumi. Kazi yetu sisi, Fikia Upeo ni kukujuza yote hayo; nasisi wenyewe tukiwa washirika wa moja kwa moja katika kuzitumia fursa zilizopo.

Hatuishii kwenye sekta ya Miliki kuu peke yake bali pia tunatoa elimu ya ujasiriamali katika ujumla wake. Karibu uambatane nasi.

Jifunze pamoja nasi

Pamoja na uwekezaji tunaoufanya kwenye sekta ya Miliki Kuu (Real Estate) na Ujasiriamali; malengo yetu ni kutoa elimu kupitia nyanja mbalimbali kama vile vitabu, semina, warsha, makongamano na kadhalika juu ya elimu ya fedha na uchumi.

Ungependa kufanya kazi nasi?

Mambo matatu yanakupa ujasiri wa kufanyakazi pamoja nasi.

24/7 Huduma kwa wateja

Wasiliana nasi kwa uhuru wakati wowote na siku zote kupitia mitandao ya mawasiliano.

Uzoefu wa zaidi ya miaka 10

Tunao uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika sekta ya Ardhi, ujenzi na ujasiriamali

Wataalam waliobobea

Tunao wataalamu waliobobea na waliojidhatiti katika kazi

Makala Mpya

Kupitia makala hizi utajifunza mambo mbalimbali. Mwisho wa kila makala utaweza kutoa maoni yako.

Je, ni jambo gani ungependa tulizungumzie?

Tunatoa ushauri kuhusu masuala ya ardhi, ujenzi wa nyumba na ujasiriamali.